Blog Archive

Monday, 14 May 2007

Mji Kasoro Bahari Morogoro-Tanzania!

1994-1999




Baada ya kumaliza elimu ya yangu ya juu niliendela kuishi Lutheran Junior Seminary nikifanya kibarua cha Kufundisha Lugha ya Kiswahili kwa wageni katika kitengo cha Shule ya Lugha na Maelekezo (Language School and Orientation- www.studyswahili.com), pia nilishikiana na rafiki yangu kaka Patrick Kaya Liganga (HollyWood Disco Sound)katika Biashara ya Muziki wa Disco pale Rock Garden na Maeneo mengine ya Morogoro, wakati huu familia yetu ikiishi katika mji wa Morogoro ambako Mama yetu aliimishiwa kikazi kwa muda katika Dayosisi ya Morogoro(KKKT). Tuliishi Maeneo ya Forest Hill na baadaye kuhamia maeneo ya Kihonda.




1998/99

Nilijiunga na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (Sokoine University Of Agriculture-SUA) katika kozi ya Kilimo kwa Ujumla (Agriculture General). Ni masikitiko yangu kusema kwamba sikufanikiwa kumaliza masomo yangu chuoni hapo nikiwa mmojawapo wa waathirika wa kushindwa kukubalika kuendelea na masomo (Victim Of Mass Failure 1999),nikiwa mwakilishi wa darasa Msaidizi(Assistant Class Representative) kipindi kigumu!
1998-nikiwa mwanafunzi wa SUA nilichaguliwa kwenda mji wa Dodoma katika Michezo ya Vyuo Vikuu (SHIMIVUTA) katika fani ya Mpira wa Kikapu, mwakilishi kutoka kambi ya Solomoni Mahalangu Mazimbu Campus!

Nilienda kuishi kwa Askofu Richard Thomas Kitale katika Kanisa La Kiinjili La Kilutheri, KKKT usharika wa Bungo nikifanya kibarua cha kufundisha na kutafsiri Lugha Kiswahili/kiingereza, wakati huu nikifanya kazi na Mchungaji Tom Foltz wa Kanisa La Kibaptisti mjini Morogoro!
Wakati huu pia nilishiriki katika timu ya mpira wa kikapu ya Morogoro Young Warriors na kuhudhuria mashindano ya mpira wa kikapu Taifa mjini Moshi, enzi za akina Kelvin Byabato, Ahmed Mayuwe, Humphrey Udoba, Joseph Mbozu, Adam Gwebe, Mkumbo Mgendi,Ey(Meneja),Bro. John Nash Prisca, Nina, sister Fatma na wengine wengi pia niliwahi kuichezea timu ya mpira wa kikapu ya Mwembeni Musoma katika mashindano ya mpira wa kikapu Taifa pale Morogoro wakati huo huo nikiwa na baadhi ya wachezaji niliwataja hapo juu tulishiriki katika mshindano ya RBA (www.basketball.com) tukiwakilisha timu ya Mbezi Beach Waves!

No comments: